Azam FC yazirudisha silaha zake kikosi
Wachezaji wawili wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC,
Nahodha Himid Mao na mshambuliaji Wazir Junior wamerejea rasmi uwanjani
kwa kuanza kufanya mazoezo mepesi mepesi baada ya kukosekana kwa kipindi
kirefu kutokana na kuwa majeruhi.
Himid
alikuwa akisumbuliwa na maumivu chini ya goti la mguu wake wa kulia
huku Junior akikabiliana na tatizo katika kifundo chake cha mguu wa
kulia na kusababisha kusababisha wapenzi wa timu hiyo kushindwa kupata
radha zao wakiwa wanalisakata kabumbu.
Aidha, Waziri Junior amesema anamshukuru Mungu kwa kuweza kurudi tena katika kikosi na kuahidi kujituma kama alivyokuwa awali.
"Kutokana na majeruhi haya ndio ilikuwa hivyo lakini tutapambana kama ilivyokuwa mwanzo, nimeu-miss sana mpira, kucheza na hata kuonyesha vile mashabiki wanataka. Lakini naamini kwa rehema za mwenyezi Mungu tutakaporejea tena basi mashabiki watafurahia vile walivyokuwa wakivisubiria", amesema Junior.
Ujio wa nyota hao umekuja wakati kikosi chao kikijiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United mchezo unaotarajiwa kupigwa katika dimba lao la nyumbani Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam siku ya Jumamosi.

No comments: