Jaji Mkuu aishauri serikali
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali
kuishirikisha Mahakama kwenye mipango yake ya uanzishaji wa maeneo mapya
ya kiutawala ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa haki kwa
wananchi.
Akizungumza
wakati wa ziara yake mjini Kigoma, Jaji Mkuu amesema mipango ya
Serikali ya uanzishwaji wa Wilaya au Mikoa uzingatie pia uanzishwaji wa
Mahakama na kwamba, Mikoa na Wilaya mpya ndizo zenye ukosefu wa Mahakama
hali inayowafanya wananchi kufuata mbali huduma za Kimahakama.
Akitolea mfano wa Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema, kutokana na Wilaya hiyo kuzunguka Mkoa, wananchi wake hulazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu zilizopo umbali wa zaidi ya kilometa 377.
Amefafanua kwamba, kupitia Mpango wa Maboresho Mahakama itaanzisha Mahakama zinazotembea yaani Mobile Courts, kwenye maeneo yote yenye changamoto kama hizo kabla ya kujenga Mahakama kwa kuwa changamoto ya upatikanaji wa huduma za Kimahakama bado ni kubwa nchini.

No comments: