Header Ads

Kufuatia hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa


Kufuatia hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa kwa viongozi 56 wa Vyama vya ushirika wilayani Masasi kwa kuwaweka ndani tarehe 23 februari, 2018 kwa makosa ya kutowalipa wakulima wa korosho kama ilivyobainishwa kwenye ripoti ya uchunguzi jumla ya shilingi milioni 39, 450,000 zimesharejeshwa na viongozi Hao.
Hayo ameyasema Leo wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Mtwara mbele ya Waziri MKuu wa Jamuhuri ya Muunganno wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Leo katika viwanja vya Ikulu ndogo Mjini Masasi katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea mkoa huo ambapo ameeleza kuwa baada ya kuona baadhi ya wakulima wa zao la korosho hawajaripwa fedha zao, mkoa uliamua kufanya uchunguzi kubaini nani anahusika na tatizo hilo na baada ya ripoti kutolewa ndipo viongozi hao wakabainika.
Byananwa amemweleza Mhe Waziri Mkuu kuwa Mkoa utaendelea kuchukua hatua ili wakulima wapate haki yao.
Aidha Byakanwa pamoja na masuala ya korosho amewasilisha Tatizo la Mji na umeme kwa mkoa wa Mtwara hasa kwa wilaya ya Masasi

No comments:

Powered by Blogger.