Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulid Mtulia amefunguka na kudai atakubaliana na matokeo yoyote
Mgombea
Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulid Mtulia amefunguka
na kudai atakubaliana na matokeo yoyote yatakayo tangazwa jioni ya leo
na Tume ya Uchaguzi Taifa (NEC) pindi zoezi la kuhesabu kura
litakapomalizika.
Mtulia
ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anafanya mahojiano ya mubashara
kutokea katika kituo alichopigia kura cha Friends Corner, Kata ya
Ndugumbi na kusema zoezi hilo linakwenda salama mpaka hivi sasa na
kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili washiriki katika zoezi hilo
ambalo ni haki yao ya kimsingi.
"Chama
changu sio cha ulalamishi na hata kama kikiona hakikutendewa haki huwa
kinafuata njia za kisheria kwa kufungua kesi Mahakamani kulalamikia
matokeo lakini tutayakubali matokeo yeyote yatakayo kuja jioni", amesema
Mtulia.
Jimbo
la Kinondoni, Siha na kata nane nchini leo yameingia katika zoezi la
kupiga kura za kuchagua wabunge watakaoweza kuwakilisha shida za
wananchi wa majimbo hayo Bungeni.

No comments: