Nyumba ya urithi haibomolewi" - Lazaro Nyalandu
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu amefunguka na
kusema kuwa nyumba ya urithi haiwezi kubomolewa na kudai kuwa tofauti
za kisiasa, ukabila na dini haiwezi kuwa sababu kwa nyumba ya urithi
kubomolewa.
Nyalandu amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook akiwa nchini
Kenya na kudai Utu, amani, haki, heshima ndiyo mshikamano wa Watanzania
wote bila kujali tofauti za kisiasa wala dini zao.

No comments: