Serikali yawapa onyo wazazi
Serikali ya Tanzania imesema itawachukulia hatua wazazi watakaobainika
kuwaweka watoto wenye ulemavu ndani badala ya kuwapeleka shule kusoma
kwa ajili ya kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa namna moja au nyingine
hapo baadae.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, alipokua akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitangali , wilayani Newala Mkoani Mtwara akiwa kwenye ziara yake mkoani humo na kusema watoto wote wana haki sawa ya kupata elimu.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kwa sasa serikali inaendelea kuboresha sekta ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira rafiki kwa watoto wenye ulemavu ili kupata elimu bora.
Msikilize hapa chini Waziri Majaliwa akiongea mengi zaidi.

No comments: