Header Ads

Somalia na AMISOM zaahidi kuimarisha ushirikiano

Somalia na AMISOM zaahidi kuimarisha ushirikiano kwenye vita dhidi ya ugaidi
Serikali ya Somalia na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM zimeeleza nia ya kuimarisha ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya ugaidi nchini humo.
Mjumbe maalumu wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kwa Somalia Bw Francisco Madeira na waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Bw Abdi Mohamed Sabriye wamesisitiza tena ahadi zao za kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab.
Bw Madeira amesema AMISOM na jeshi la Somalia ni nguvu moja, na wana lengo la pamoja la kupambana na kundi la Al-Shabaab. Bw. Sabriye amesisitiza kwamba vikosi vyote vya usalama vinavyofanya operesheni nchini Somalia, ni lazima visaidiane na kuungana mkono.

No comments:

Powered by Blogger.