Sugu na mwenzake watupwa jela
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa
Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamekutwa na
hatia katika ya kesi inayowakabili na kutakiwa kwenda jela miezi mitano.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya HakimuMkazi Mbeya,
Michael Mteite amesema kwamba washtakiwa hao wanapaswa kwenda jela
kutokana na makosa waliyoyatenda katika mkutano wao wa hadhara ambao
ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya.
Kwa upande wa Washtakiwa Wakili Peter Kibatala aliyekuwa anamuwakilisha Sugu pamoja mwenzake aliiyomba mahakama hiyo iwapunguzie adhabu wateja waken kutokana na majukumu yanayowakabili ikiwepo la Sugu la kuwawakilisha wananchi bungeni.
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

No comments: