Header Ads


Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutojihusisha na maswala ya kisiasa katika utendaji wao wa kazi ili kuandika habari za ukweli na usahihi.
Hayo yamesemwa na Naibu Wziri  JULIANA SHONZA kwaniaba ya Waziri wa Habari,Tamaduni,sanaa Na Michezo katika maadhimisho ya siku ya redio duniani ambayo kitaifa yamefanyikia Mjini DODOMA.
Naibu waziri amesema waandishi wa habari wanajukumu la kufikisha habari kwa jamii ili kulinda amani,na upendo kwa kujali utu wa mtu.
Amesema vyombo habari vina nafasi kubwa katika jamii na kama vikitumika kwa mengo sahihi itasaidia kuiunganisha jamii na serikali.
Maadhimisho ya siku ya redio duniani kitaifa yamefanyika Mjini DODOMA huku yakibebwa na kaulimbiu ya ‘redio na Michezo’ ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu waziri wa Habari, Utamadunii sanaa na Michezo Mh JULIANA SONZA kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dr. HARRISON MWAKYEMBE.

No comments:

Powered by Blogger.