Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganno wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa kata ya Chiungutwa Halmashauri ya wilaya ya Masasi leo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganno wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa kata ya Chiungutwa Halmashauri ya wilaya ya Masasi leo ikiwa ni ukamilishaji wa ziara yake ya kikazi wilayani Masasi ambapo amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitolea ufafanuzi.
Waziri Mkuu amewaeleza wananchi kuwa serikali inatambua kuwa korosho ndio zao kuu la kiuchumi na inafanya jitihada kubwa kusimamia zao hilo, hivyo wananchi wapande miche mipya ya mikorosho ili kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza uzalishaji utakaofanya mkulima apate kupata kipato kikubwa zaidi.
Kutokana na viongozi wengi wa Vyama vya ushirika kutokuwa waaminifu,
Waziri Mkuu amewaeleza wananchi kuchagua viongozi waaminifu ili waweze
kusimamia fedha zao vizuri kwani kwa sasa serikali inaendelea kuchukua
hatua kwa viongozi wa sasa waliosababisha baadhi ya wakulima kutolipwa
fedha zao ambapo kwa msimu wa 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni
1,241,294, 778 hazijalipwa.
Aidha Waziri Mkuu amemwagiza Mragisi wa Mkoa wa Mtwara kukigawa chama Kikuu cha Ushirika (MAMCU) ili kiweze kuhudumia wakulima kwa ufanisi zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo Chama hicho kinashindwa kuwasimamia wakulima ipasavyo kutokana na kuwa na eneo kubwa la kusimamia.
Ifahamikekuwa chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU kinasimamia wakulima wa Tunduru, Nanyumbu, Masasi na Mtwara hivyo imekuwa vigumu kufuatilia maslai ya wakulima ipasavyo.

No comments: