"Akipata Seif tumepata sote" - Prof. Lipumba
Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba
amesema CUF sana Katibu mkuu wake, Seif Sharif Hamad kwa kudhani kuwa
kama angepata yeye basi wamepata wote kumbe ni tofauti kitu ambacho
waliwakosea Wazanzibar.
Prof. Lipumba
ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao cha kwanza cha kawaida cha
Baraza Kuu la Uongozi la CUF kilichofanyika katika makao makuu ya chama
hicho, maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa hali ya kumdekeza Seif imesababisha CUF kushindwa kupata viongozi watakaoingia katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na kutokuwepo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
“CUF tumemdekeza kwa muda mrefu na zile nyimbo tulizokuwa tukiimba ya kuwa akipata Seif tumepata sote zilikuwa zimemuingia kichwani kwelikweli na yeye alitafsiri kuwa akikosa Seif tumekosa sote, matokea yake tumekosa kuwa na uwakilishi katika Baraza la Uwakilishi jambo ambalo limetuathiri kisiasa hasa Zanzibar. Hili kosa kubwa tuliowakosea Wazanzibari” amesema Prof. Lipumba.

No comments: