ATCL Yasitisha Safari za Songea- Dar es Salaam
Kampuni
ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itasitisha safari kati ya Dar es Salaam na
Songea kuanzia Machi 31, mwaka huu, kutokana na ubovu wa njia ya kurukia
ndege katika uwanja wa Songea.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
Ladislaus Matindi, safari hizo zitarudishwa baada ya kukamilika kwa
matengenezo makubwa ya uwanja huo yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
“Kusitishwa
kwa safari za Songea kutaathiri pia safari za Mtwara kwa kipindi kifupi
kutokana na sababu za kibiashara wakati ATCL ikitathmini njia mbadala
ya kuhudumia kituo hiki peke yake,” imesema taarifa.
Alisema
ATCL inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana
na uamuzi huo kwani usalama wa wateja ndio kipaumbele cha kampuni hiyo.

No comments: