Bifu mpya mjini, wasanii watifuana
Wasanii Nikki Mbishi na Moni
wa Centrozone wametupiana maneno baada ya hivi karibuni Nikki kusema
kuwa kundi jipya la Moni linalofahamika kama MOCO ni lakupita tu wala
haliwezi kufika mbali.
Akiongea
kupitia eNEWZ Moni amesema kwamba anamshangaa sana Nikki amekuwa ni
mtu wa kulalamika na lawama huku akiongeza kuwa siku hizi hata kazi za
Nikki hazioni zaidi anasikika akiwa analalamika tu.
Moni amesema yeye na kundi lake hawafanyi Rap ya kilingeni bali anafanya Rap ya biashara hivyo hayo maneno ya Nikki wala hayamsumbui kwasababu tayari wamefanya kazi nyingi na wanashukuru Watanzania wamewapokea.
Kwa upande mwingine Moni ambaye anatamba na ngoma yake mpya ya Nichum amesema kinachomsumbua Nikki ni uzoefu wake wa kuvunjikiwa na kundi kutokana na uzembe wake huku akimshauri kuwa afanye kazi kwa bidii kwa kuwa anamizizi mizuri na nimuandishi mzuri hivyo asimamie sanaa yake kwanza.

No comments: