Chelsea yapata pigo
Klabu ya soka ya Chelsea
kuelekea mchezo wake wa ligi kuu ya England dhidi ya Tottenham, huenda
ikamkosa mlinda mlango wake namba moja Thibaut Courtois baada ya kuumia
akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji.
Mchezaji
huyo amelazimika kuondolewa kwenye kikosi cha Ubelgiji
kitakachokabiliana na Saudi Arabia siku ya Jumanne Machi 27 kwenye mechi
ya kirafiki ya kalenda ya FIFA kwa mwezi Machi.
Kabla ya Courtois kuumia kocha wa Chelsea Antonio Conte hivi karibuni alithibitisha kuwa nyota huyo anasumbuliwa na misuli, tatizo ambalo lilianza baada ya mchezo wa robo fainali ya kombe la FA.
Nafasi ya Coutois kwenye mchezo huo inatarajiwa kuzibwa na Simon Mignolet wa Liverpool au Koo Casteels na Matz Sels ambao ndio chaguo jingine ndani ya kikosi hicho cha kocha Roberto Martinez.
Chelsea itakuwa nyumbani kucheza na Tottenham Jumapili ijayo. Chelsea tayari inashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na 56 huku Tottenham wakiwa katika nafasi ya 4 wakiwa na alama 61.

No comments: