Diego Costa awachana Argentina kuhusu Messi
Mshambuliaji wa Hispania
Diego Costa amefunguka na kuwataka mashabiki wa soka nchini Argentina
kumshukuru Mungu kwaajili ya Messi na sio kumkosoa mchezaji huyo.
Maneno
hayo ya Costa yamekuja ikiwa ni masaa machache yamepita tangu Hispania
itoe kichapo cha mabao 6-1 dhidi ya Argetina kwenye mchezo wa kirafiki
uliopigwa Wanda Metropolitano.
''Nadhani leo wameona wenyewe bila Messi wao ni kina nani, hivyo wanapaswa kuheshimu mchango wa Messi'', amesema Costa kwenye mahojiano baada ya kurejea kwenye timu yake ya Atletico Madrid mapema leo.
Costa pia ameongeza kuwa, "Mchezaji kama Messi hapaswi kuhukumiwa, unapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa yupo kwenye timu yako hata kama hajafanya vizuri na timu ya taifa lakini kuwa naye kuna na kumkosa kunatofauti kubwa''.
Katika mchezo wa jana usiku Costa alifunga bao moja huku nyota mwingine Isco akifunga hat-trick. Costa amerejea kwenye klabu yake ya Atletico Madrid baada ya kushindwana na klabu ya Chelsea.

No comments: