HASIRA ZA WANANCHI:
Wananchi wenye hasira kali wamejichukulia sheria
mkononi kwa kulichoma gari aina ya Lori baada ya dereva wake kumgonga na
kufa papo hapo muuguzi wa Zahanati ya Kaseme wilayani Geita.
Tukio hilo limetokea Jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika Bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina Paulo Talafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusulika na kifo hicho.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi na walipojaribu kupishana na gari jingine ndipo likawagonga na mama huyo kuumia kuanzia sehemu ya kiuno hadi miguuni na kusababisha utumbo kutoka nje.

No comments: