"Hii vita siyo ya CHADEMA"- Lema
Lema
ametoa kauli hiyo leo (Machi 28, 2018) wakati alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kikao cha
Kamati Kuu kilichoitishwa kwa dharula ili kuweza kutoa msimamo wa chama
chao kutoka na viongozi wao wa nafasi za juu akiwemo Freeman Mbowe
kulala Segerea kutokana na kunyimwa dhamana katika kesi zao zilizosomwa
jana.
"Muelewe tu kwamba hii vita sio ya CHADEMA bali hii vita ni demokrasia hata sisi tukisema tunaiacha siasa vita hii itaendelea tu. Haya mashaka tunayavumilia kwasababu ya msingi ya vizazi na nchi yetu, ndio sababu kubwa tunavumilia mateso na udhalilishaji. Lakini nafikiri sasa inatosha",amesema Lema.
Pamoja na hayo, Lema ameendelea kwa kusema "viongozi watakwenda kushauriana na Mwenyekiti Mbowe kule magereza kwamba kesho wakinyimwa dhamana basi tutaitisha mkutano na waandishi wa habari na baada ya hapo ndipo tutajua kama ni kufungulia maji au laa...
"yeyote aliyetusaidia kwa namna yeyote ile hatutasita kumuweka wazi kwa wananchi ili ijulikane sasa hakuna namna ya kuendelea hivi tunavyo kwenda kwasababu kuwa weka watu ndani na kuwanyima dhamana ni sawa na kukiweka chama kizima ndani".
Kwa upande mwingine, Lema amedai hayo mambo yanayoendelea kutokea hasa katika chama chao anakijua vizuri huku akisisitiza kuwa kuna asilimia kubwa kesho viongozi wao wa nafasi za juu Chadema watakosa dhamana kutokana na huo mkakati hautoki katika ofisi ndogo kama watu wanavyofikiria.

No comments: