Kamati ya Utekelezaji ya
Umoja wa Vijana wa CCM iliyokutana kwa dharura mchana huu chini ya
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kheir Denis Jemes imetengua uteuzi
wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Jokate U. Mwengelo
kuanzia leo
Taarifa
hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa
Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika
nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.
Kikao hicho kilichomtengua Jokate kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Kheri Denis James (MCC) katika
ukumbi wa secretariet White house Mjini Dodoma lakini bado hawajaweka
wazi sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo.
No comments: