Header Ads

Jopo la madaktari wa PSG na Brazil lafanya maamuzi juu ya Neymar

Jopo la madaktari wa PSG na Brazil lafanya maamuzi juu ya Neymar
Baada ya jopo la madaktari wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa na jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Brazil washirikiana kumfanyia uchunguzi wa kina mwanandinga Neymar, leo wamefikia makubaliano ya kumfanyia upasuaji baada ya kuona hakuna njia mbadala ya kutatua tatizo lake zaidi ya upasuaji.
Madaktari hao wamethibitisha kuwa Neymar amevunjika mfupa wa mguu wa kulia karibu na enka siku ya jumapili dakika ya 77 ya mchezo dhidi ya Marseille iliyomalizika kwa PSG kuibuka mshindi wa magoli 3-0. Upasuaji huo utafanyika wiki hii nchini Brazil.

No comments:

Powered by Blogger.