Header Ads

Kitokololo atoa siri ya Kanal Top

Msanii wa muziki wa bolingo mwenye asili ya Kongo, Kitokololo ameweka wazi juu ya anachokifahamu kuhusu mwanamuziki mwenzake Kanal Top, ambaye tetesi zinasema kuwa alinyongwa baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Kitokololo amesema hana taarifa zaidi kuhusu Kanal Top na hana mawasiliano naye kwa zaidi ya miaka minne sasa, lakini akiuliza ndugu zake wanasema yupo na anafanya mambo yake kama kawaida.
“Kanal Top mi mi nilisikia amesafiriri kwenda kufanya mambo yake, kuhusu mambo hayo mimi sijafuatilia sijajua zaidi, nakumbuka aliniambia nasafiri naenda nje naenda kufanya muziki wangu huko, kuhusu  hayo memgine nilikuwa sijajua, naulizaga ndugu zake wanasema yupo anafanya mambo yake kama kawaida, wananiambia hivyo lakini mengine sijajua”, amesema Kitokololo.
Tetesi za msanii huyo maarufu wa muziki wa bolingo kunyongwa zilifuatia baada ya barua zilizokuwa zikitumwa na watanzania ambao wamefungwa China wakielezea hali zao huko, lakini hakukuwa na mtu yeyeote aliyezungumzia kuhusu msanii huyo, ambaye mpaka sasa ni zaidi ya miaka minne hajulikani alipo baada ya taaarifa za kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China.

No comments:

Powered by Blogger.