Mahakama yawafutia 44 kesi, Wabunge wang'ang'aniwa
Washtakiwa 44 kati ya 57 wa
kesi ya kuchoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji cha Sofi wilayani
Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa mashtaka na kuwa huru, huku wabunge
wa CHADEMA wakipamgiwa tarehe ya kusomewa maelezo ya awali mwezi ujao.
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera aliwasilisha ombi la kuwafutia mashtaka washtakiwa hao 44 kwa kile walichodai kuwa hawana ushahidi wa nguvu utakaowatia hatiani washtakiwa hao.
Mawakili upande wa utetezi umeweka wazi kuwa wanajiandaa kukabiliana na ushahidi utakaotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya wabunge hao na wengine 11.
No comments: