Header Ads

Mambo bado si shwari kwa Samatta

Tangu nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta apone majeraha na kurejea dimbani, mambo bado hayajakaa vizuri baada ya jana kuanzia benchi huku timu yake ya KRC Genk ikipoteza.

Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania kwenye mchezo huo wa jana, ligi kuu ya soka ya Ubelgji alingia dakika ya 78, wakati ambao tayari timu yake ilikuwa nyuma kwa mabao mawili dhidi ya Gent.
Baada ya kuingia akichukua nafasi ya kiungo Alejandro Melero Samatta aliongeza nguvu katika kikosi cha Genk ambayo ilifanikiwa kufunga bao moja dakika ya 87 na kufanya mechi kumalizika kwa 2-1.
Mchezo huo wa jana ulikuwa ni wa 78 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo amefanikiwa kufunga mabao 22.
Baada ya mechi hiyo ambayo Genk ilikuwa nyumbani, timu hiyo imesalia na alama 44 katika nafasi ya tano huku Gent ikifikisha alama 50 katika nafasi ya nne.

No comments:

Powered by Blogger.