Mbunge akamatwa kwa kupanga mauaji
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la
Laikipa Mshariki nchini Kenya Mathew Lempurkel, amekamatwa tena na
polisi nchini humo, baada ya kuachiwa siku ya tarehe 12 machi, kwa
tuhuma za kupanga mauaji.
Kwa
mujibu wa Polisi wa Laikipa Kaunti Kamanda Simon Kipkeu, bwana
Lempurkel ambaye alikuwa mbunge kupitia chama cha ODM, atafikishwa
mahakamani baada ya wapelelezi kukamilisha taarifa zao.
Lampurkel alikamatwa baada ya kutishia kukichoma moto kituo cha polisi cha Rumuruti, kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu mwezi Julai, 2016.
Mahakama iliamua kuwa Lampurkel ana kesi ya kujibu juu ya vurugu alizofanya, na kisha kukamatwa tena kwa tuhuma za kupanga njama hizo za mauaji.

No comments: