Mkapa ataka mjadala wa Kitaifa
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Mh. Benjamini William Mkapa amesema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa
kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali
kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Mkapa
ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma
wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu
hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu na kumuaga Makamu Mkuu wa chuo
hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula.
Mhe.Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi ama ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana.

No comments: