Mzazi mwenzie Alikiba afunguka kuhusu matunzo
Baada ya kusambaa tetesi
kupitia mitandao ya kijamii kuwa msanii Alikiba ni kati ya wasanii ambao
hawatunzi watoto wake moja ya mwanamke ambaye amezaa naye mtoto wa
kiume Mama Unju amefunguka na kuweka wazi juu ya sakata hilo.
Aidha Mama Unju amekwenda mbali zaidi na kutoa ushauri kwa wanawake hao ambao wamezaa na Alikiba na kuwataka kutotumia watoto wao kurudisha mapenzi kwa Alikiba au kutumia watoto wao hao ili waweze kusaidiwa ukoo mzima bali kila mmoja akomae na kupamba na hali yake kama ambavyo yeye alikubaliana na hali baada ya wao kutengana.
Mbali na hilo mzazi mwenzie na Alikiba alimpa ushauri Alikiba na wanaume wengine kuwa wanatakiwa kuangalia aina ya wanawake ambao wanaamua kuwa nao kwenye mahusiano kwani si kila mtu anaweza kuwa na nia nzuri na kuwa wapo watu wengine hawajielewi na hawajui kile wakifanyacho.

No comments: