Rais Magufuli awape neno wanawake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
Machi 8, 2018 katika siku ya wanawake duniani amefunguka na kuwapongeza
wanawake wote wa Tanzania na kuwatakia kheri katika siku yao hii muhimu.
Magufuli
ametoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kuwa
wanawake wamekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii na kusema daima
ataendelea kuwaheshimu
"Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu" alisema Rais Magufuli

No comments: