Rais Magufuli kuzindua magari
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Machi 26, 2018 anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 ambayo yatakuwa yakitumika
kusambaza madawa vijijini na mjini.
"Mageuzi Sekta ya Afya yanaendelea, usikose hafla ya kupokea magari mapya 181 kufikisha dawa na vifaa tiba zaidi mijini na vijijini" alisema Dkt Abass
Mbali na hilo Rais Dkt John Magufuli, Mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa leo Machi 25, 2018 wameshiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la St. Peters Oysterbay jijini.

No comments: