Header Ads

SIMBA YAENDELEA KUWAWINDA AL MASRY SC, NI MAZOEZI MWANZO MWISHO

Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi jioni hii katika Uwanja wa Boko Vetarani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.

Simba wanajiandaa na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC kutoka Misri. Mchezo huo utafanyika huko Misri, Machi 17 2018.

Mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2, hivyo Simba watalazimika kwenda kushinda ugenini ili wapate nafasi ya kusonga mbele.

Taarifa kutoka ndani ya wekundu hao wa Msimbazi, zimearifu kuwa kikosi chao kitaondoka nchini Jumatano ya wiki hii kuelekea Port Said, Misri, kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.

No comments:

Powered by Blogger.