Trump akubali mualiko wa kukutana na Kim Jong Un
Rais
Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini
Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu,na
hivyo kuweka historia kufuatia kutokuwepo rais wa Marekani ambaye
amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.
Hata
hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa,na
pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim
Jong Un lakini bado vikwazo vitasalia pale pale.
Tangazo
hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un,limetolewa
na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha
barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.
Kim
pia amekubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na majaribio yake ya
makombora,msimamo ambao ni tofauti na aliokuwa nao rais huyo Kim Jong
Un.
Hatua
hii iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un kulegeza msimamo ni matokeo ya
mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita ujumbe wa Korea
Kusini kukutana na kiongozi huyo.
No comments: