Header Ads

UKAWA yalia na Serikali juu ya kina Mbowe



Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro ameituhumu serikali kuihujumu mahakama kwa kushindwa kuwafikisha viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama jinsi ambavyo mahakama ilielekeza Machi 27.
Mtatiro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari nje ya ya Mahakama baada ya dhamana ya viongozi hao sita wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe kushindwa kukamilika kutokana na viongozi hao kushindwa kufikishwa mahakamani kutokana na gari la Magereza kuharibika.
“Tunatambua mpaka sasa Mwenyekiti mwenza UKAWA Freeman Mbowe na wenzake bado wapo gerezani, UKAWA inalaumu kwa nguvu zote kitendo cha Serikali na Management ya Magereza kushindwa kuwaleta Washtakiwa Mahakamani, hii ni moja ya hujuma kubwa sana” Mtatiro.
Amesema kuwa hujuma hiyo inaathiri  haki ya utendaji wa mahakama na mazingira ya upataji haki ya wananchi.
Mbali na hayo Mtatiro ameongeza kuwa anafahamu kuwa Serikali ilikuwa na magari pamoja na mafuta ya kumsafirisha usiku wa manane mwanafunzi Abdul Nondo mpaka  Iringa lakini serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwatoa kina Mbowe kutoka Segerea mpaka Kisutu na kushauri kwamba ni muhimu masuala yanapokuwa yamefika mahakamani yaachwe mahakamani.
Pamoja na hayo Mtatiro ameishukuru Mahakama kwa kutenda haki kwa viongozi hao na kuiomba indelee kuwa imara ili wananchi wapate haki.

No comments:

Powered by Blogger.