Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi
Kamati ndogo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia vitendo vya utesaji na
unyanyasaji 'SPT' imeamua kurejea nchini Rwanda baada ya kusimamisha
uchunguzi huo Oktoba 2017, ingawa tarehe ya kurejea huko haijatangazwa
mpaka hivi sasa.
Ziara
hiyo iliamuliwa wakati wa kikao cha SPT kilichofanyika mjini Geneva
Uswisi ambapo kamati hiyo vilevile imeamua kudurusu orodha ya mataifa
ambayo hadi sasa yameshindwa kuunda chombo cha kitaifa kinachochunguza
uzuiaji katika kipindi cha miaka minne baada ya kuudhinisha.
Kamati ndogo ya kuzuia utesaji-SPT inauwezo kufanya ziara yoyote ya kushtukiza kwa eneo lolote ambapo haki za watu zikiwa zinakiukwa katika nchi ambayo iliidhinisha itifaki ya mkataba wa kuzuia utesaji.
Vituo hivyo vinaweza kuwa ni magereza, vituo vya polisi, vituo vya kuwazulilia wahamiaji, vituo vya kuwashikilia watoto, vifaa vya kudodosa, na hospitali za watu walio na ulemavu wa akili.

No comments: