Uwoya chanzo cha Dogo Janja kuwa 'mwanamke'
Msanii wa muziki wa kizazi
kipya Dogo janja ambaye sasa hivi ameachia video ya wimbo wake mpya wa
'Wayu wayu' na kuacha gumzo kwa mashabiki kwa kuvaa uhusika wa mwanamke,
na kusema kuwa mke wake ndiye alimfanya awe hivyo.
Akizungumza
kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema mke wake
ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Irene Uwoya, ndiye alianza
kumfanyia make up wakiwa mapumzikoni Zanzibar, na kumvalisha vitu vya
kike, ndipo walipopata idea ya kufanya video akiwa kama mwanamke.
“Mke wangu kabla sijaanza kushoot alianza kunifanyia make up na kunivesha vesha tulipokuwa vacation (mapumzikoni) Zanzibar, akawa ananicheka, mpaka siku tunaenda kushoot ile make up ilibidi anifanyie yeye lakini ilitokea dharula hakuwepo, akaniambia niende kwa mtu anifanyie make up ya nude mimi hata siijui, hata lile wigi alinipa mke wangu na mimi nikapita nalo”, amesema Dogo Janja.
Kitendo cha Dogo Janja kuigiza kama mwanamke kimeonekana kuwakwaza watu wengi wakisema sio kitu kizuri mwanaume kuvaa hivyo na kujipodoa kama mwanamke, lakini kwa upande wake amesema ilikuwa ni ubunifu kwa lengo la kuboresha kazi.

No comments: