Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kupitia baraza kuu la uongozi Mkoa wa Morogoro
limemvua James Mkude nafasi aliyekuwa akiishika ya Mwenyekiti wa
Manispaa ya Morogoro kutokana na tuhuma za kujihusisha na matukio yaliyo
kinyume na katiba ya chama hicho.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo ambaye pia ni
Mbunge wa jimbo la Mlimba Bi. Suzani Kiwanga na kusema hatua hiyo
imekuja baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizo wasilishwa ndani ya chama
hicho ingawa ni tuhuma binafsi zinazomkabili mwenyekiti huyo
aliyesimamishwa na kwamba hazihusiani na chama.
Akitoa maadhimio ya wajumbe wa baraza la uongozi la chama hicho mkoa
wa Morogoro waliokutana kujadili muenendo wa mwenyekiti huyo, Bi. Suzani
amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 2006 toleo la
mwaka 2016 kifungu cha saba pamoja na maadili ya uongozi kinatoa
mamlaka kwa baraza hilo kumsimamisha mtu yeyote atakae kiuka maadili ya
kinidhamu ya chama hicho.
No comments: