"Mkuu wa Mkoa ana nguvu kuliko waziri" - Mwakajoka
Mwakajoka
amesema hayo bungeni wakati akichangia hoja na kusema kuwa saizi
utawala bora haupo kabisaa na kwenda mbali na kudai kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kinataka kuvunja muungano ambao ulihasisiwa na viongozi
wa taifa Mwalimu Nyerere pamoja na Karume na ndiyo maana viongozi
wamekuwa kimya pindi wabunge wanapotumia lugha za kuudhi na zihaka kwa
watu wa Zanzibar.
"Katika nchi hii sasa utawala bora hakuna kabisa yaani huwezi kuamini saizi katika nchi hii Waziri anaweza kumuaagiza Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya tena kwa barua lakini viongozi hao wasitekeleze kabisa hicho walichoagizwa hii imekuwa nchi ya aina gani sasa. Yaani sasa hivi Mkuu wa Wilaya ana nguvu kuliko waziri, Mkuu wa Mkoa ana nguvu kuliko waziri. Kwenye mji wetu wa Tunduma kuna mgogoro ambao upo umekaa kwa muda mrefu sana kuanzia mwaka jana mpaka leo waheshimiwa madiwani hawajakaa vikao kwa sababu ya amri ya Mkuu wa wilaya, sasa Mkuu wa wilaya ana mamlaka gani ya kuzuia baraza la madiwani katika maeneo yetu" alihoji Mwakajoka
Kuhusu suala ya lugha za kuudhi na kebehi kwa watu wa Zanzibar zinazotolewa na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwakajoka amesema kuwa hilo ni lengo la Chama Cha Mapinduzi kuvunja muungano huo kitu ambacho si kizuri.
"Inaonesha kabisa CCM wanataka kuvunja Muungano kwa sababu wanaonyesha kabisa hawathamini kazi walizofanya baba wa taifa pamoja na Karume huwezi kuamini yapo matamko mabaya yanayotokea hapa kwa ajili ya kubeza kila siku, watu tunasikia kila siku lakini hatujawahi kusikia hata siku moja kiongozi mkubwa wa serikali, wala Spika wa Bunge hili, Naibu Spika wamekemea jambo hili hili jambo ni hatari sana, watu wana lalamika ndani ya bunge hili na sisi tumeungana kama Watanzania kwa sababu ya nchi mbili Zanzibar na Tanzania bara hivyo suala la muungano ni vizuri tukaheshimiana ndani ya bunge hili lakini pia tukawaheshimu wananchi wote wa Tanzania bara na visiwani" alisisitiza Mwakajoka

No comments: