Muhimbili yatoa idadi ya watoto waliozaliwa
Jumla ya watoto 7 wamezaliwa
siku ya leo Aprili Mosi, 2018, ambayo ni sikukuu ya pasaka, katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Taarifa
hiyo imetolewa na ofisi ya mahusiano ya hospitali ya Muhimbili, ambapo
imeeleza kwamba watoto hao waliozaliwa wanne ni kike, huku wakiume
wakiwa watatu, na wazazi sita wakiwa wamejifungua kawaida na mmoja kwa
upasuaji.
Mama na watoto hao wote wapo salama na wanaendelea vizuri hospitalini hapo.
Mama na watoto hao wote wapo salama na wanaendelea vizuri hospitalini hapo.
No comments: