Ripoti ya CAG yazua taharuki kwa Mawaziri
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti Naghenjwa Kaboyoka wa PAC na Vedasto Ngombale
ambaye ni mwenyekiti wa LAAC, wakati walipokuwa wanazungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dodoma baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Mussa Assad, kuwasilisha ripoti ya
ukaguzi iliyoishia Juni 30, 2017 kwa waandishi wa habari mjini Dodoma
wiki iliyopita kisha kuanza kuonekana kwa baadhi ya Mawaziri kujibu
ripoti hiyo nje ya Bunge.
"Mawaziri sita ambao wamejibu hoja za CAG kupitia kwa waandishi wa habari wanakiuka sheria na hawapaswi kujibu badala yake wanaotakiwa kufanya hivyo ni makatibu wa wizara wenye wajibu ambao ndiyo wanaitwa na kuhojiwa na kamati husika", wamesema wenyekiti hao.
Hii ni kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge nchini, hoja zinazotolewa na CAG zimekuwa zikijibiwa na Mawaziri kabla hazijafikishwa mbele ya Wabunge.

No comments: