TFF yawaweka wazi ratiba ya nusu fainali
Hayo
yamewekwa wazi na Afisa Habari wa TFF, Cliford Mario Ndimbo wakati
alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na
kusema nusu fainali ya kwanza itachezwa siku ya Ijumaa Aprili 20,2018
ikiwakutanisha Stand United ya Shinyanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa
Sugar ya Morogoro kwenye uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga.
Aidha, Ndimbo amesema timu ya Singida United watawakaribisha JKT Tanzania kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa katika dimba la Namfua siku ya Jumamosi Aprili 21,2018.
Kwa upande mwingine, Ndimbo amesema washindi kwenye nusu fainali hizo watacheza mchezo wa fainali Mei 31, 2018.

No comments: