Waziri ashauri kuhusu maandamano
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista
Mhagama amefunguka na kutoa ushauri kuhusu suala la maandamano na kusema
kuwa mtu yoyote ambaye ana ratibu maandamano lazima afuate sheria hata
kama maandamano yanatambulika kikatiba.
"Suala la maandamano katika nchi yetu ya Tanzania linaratibiwa na sheria za usalama ndani ya nchi chini ya vyombo vya usalama hasa polisi na Katiba haiwezi kuchukuliwa kwamba ni kigezo cha kuviruhusu vyama kufanya maandamano bila kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa, ninaomba sana Watanzania wote na niviombe vyama vyote vya siasa katika nchi yetu ya Tanzania wahakikishe wanazingatia sheria. Katiba yetu imeruhusu maandamano lakini maandamano yameratibiwa kisheria na kama yameratibiwa kisheria lazima tuhakikishe kwamba tunazingatia sheria katika kuratibu maandamano nchini kwetu Tanzania"
Jenista Mhagama aliendelea kutoa maelezo kuhusu masuala ya maandamano
"Labda niulize swali moja tukiamka hapa siku moja asubuhi na kila mtu ameamua kuandamana wakulima, wafanyakazi yaani kila mtu aamue tu kuandamana kwa sababu tu Katiba imesema nadhani itakuwa siyo sawa na nichukue nafasi hii kuviomba vyama vya siasa kuheshimu Katiba na sheria katika kutekeleza wajibu wao na siyo kuvunja sheria za nchi yetu Tanzania"

No comments: