Header Ads

Azam FC yakusudia kuipoteza Yanga mazima ?



Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, usiku wa leo itashuka katika dimba lake la nyumbani la Azam Complex kuvaana na Majimaji ya Songea kwenye michuano ya ligi kuu wakiwa wanazisaka alama tatu za mchezo zitakazowaweka imara kwenye nafasi ya pili ya ligi.
Wakati Azam FC imejipanga kupata matokeo mazuri katika mchezo wake huo ili kuendelea kufukuzana na Yanga yenye alama 48 kuwania nafasi ya pili kwenye msimamo, Majimaji yenyewe itakuwa ikijaribu kusaka pointi iweze kujinusuru kushuka daraja msimu huu kwani hadi sasa ipo nafasi ya 13 ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 24 ikiizidi pointi mbili Njombe Mji inayoshika mkia.
Pamoja na hayo, tayari benchi la ufundi la Azam FC linalosimamiwa na Kocha Msaidizi Idd Cheche na Kocha wa timu ya Azam B, Meja Abdul Mingange, baada ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba kwenda kusoma, limeshawaambia wachezaji wao juu ya umuhimu wa mechi zilizobakia katika kuhakikisha inashinda zote ili kujiweka pazuri kwenye msimamo.
Kwa upande mwingine, Azam FC itaendelea kuwakosa wachezaji wake mabeki Yakubu Mohammed, Swaleh Abdallah, Daniel Amoah, ambao ni majeruhi.
Wachezaji wengine walioukosa mchezo uliopita kutokana na kuwa wagonjwa, Nahodha Msaidizi Agrey Moris, kipa Razak Abalora, winga Enock Atta na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, tayari wameanza mazoezi na wenzao kujiandaa na mchezo huo na litabakia ni jukumu la benchi la ufundi kuona kama wanafaa kucheza.

No comments:

Powered by Blogger.