Lwandamina atambulishwa klabu mpya
Lwandamina
ambaye ameifundisha Yanga kwa misimu miwili, kesho ataanza rasmi kazi
na Zesco United ambayo itakuwa dimbani kucheza na Mbabane Swallows ya
Swaziland kwenye uwanja wa Ndola, Zambia.
Lwandamina ameondoka Yanga mwezi uliopita baada ya kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kurejea timu yake ya zamani, Zesco ambayo pia aliwahi kuifikisha katika hatua za juu katika michuano ya vilabu Africa.
Kwa upande mwingine Barani Africa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa inaanza rasmi leo kwa mechi tatu kuchezwa katika nchi za Botswana, Misri na Algeria.
Nchini Botswana wababe wa Yanga kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Township Rollers watawakaribisha KCCA ya Uganda wakati Al Ahly watawakaribisha ES Tunis ya Tunisia huku MC Alger watakuwa wenyeji wa Difaa Hassan El- Jadida ya Morocco.

No comments: