Header Ads

Somalia kuanzisha kituo cha mabadilishano cha Internet IXP




Serikali ya Somalia imetangaza kuwa imepanga kuanzisha kituo cha kwanza cha mabadilishano cha mtandao wa internet IXP mjini Mogadishu, ili kusaidia kuimarisha huduma za kidigitali nchini kote.

Waziri wa posta, mawasiliano ya simu na teknolojia wa Somalia Bw Abdi Ashur Hassan, amesema kuanzishwa kwa kituo hicho ni hatua muhimu katika kujenga miundombinu ya Tehama ya Somalia, ambayo itaimarisha huduma za kidigitali zinazotolewa na mashirika ya kienyeji kwenye biashara, elimu, afya na huduma za serikali.

Ameongeza kuwa serikali inataka miundombinu hiyo imilikiwe na kusimamiwa na wadau, ambao wanatakiwa kutoa mfumo bora wa usimamizi na kuunda tume ya mpito ya kuendesha kituo hicho.

No comments:

Powered by Blogger.