Kampuni inayotoa huduma
katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha
usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana
kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana
na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na
kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu
ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha
usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.
"Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara,
Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili,
Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea
mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus
Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu
ambao utajitokeza kwa namna moja ama nyingine.
No comments: