Waziri wa fedha amekiri serikali ni mufilisi -Mdee
Halima
Mdee alisema hayo bungeni wakati akichangia hoja katika bajeti ya
Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa inashangaza kuona Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inatengewa fedha na zinapatikana fedha
ili hali Wizara zingine inaonekana fedha hakuna.
"Kwanza nashukuru Waziri wa Fedha amekiri serikali yake ni mufulisi haina pesa, haiwezekani mnatuambia mnakusanya zaidi ya Trilioni 1.3 kwa mwezi na mmevunja rekodi ya serikali zote zilizopita lakini bajeti yetu sisi tunapanga kutokana na vyanzo vyetu halafu mnatuambia leo kumbe uwezo wenu ni kutekeleza asilimia 22 tu, Waziri wa Fedha anatuambia hapa kwamba serikali haina uwezo wa kutoa pesa lakini Wizara ya Ujenzi imepewa bajeti zaidi ya asilimia 70 ya utekelezaji sasa hapa tunajiuliza hivi uhai wa binadamu wa kupata maji na hizo barabara zenu kipi ni muhimu? Alihoji
"Unasema huna pesa nimetoa pendekezo tutoe shilingi 50 tuongeze tuweke kwenye mfuko mnakataa sasa kama mnakiri mnashindwa kutumia pesa vizuri kwanini mnakuja kutuomba tena Bilioni 673, yaani Bunge tuwapitishie Bilioni 673 za maji huku unajua kuwa bajeti hewa, mnashindwa kwenda kuisimamia" alisema Halima Mdee.

No comments: