Header Ads

“Jina la simba liheshimike”- Kocha Pierre

Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Pierre Lechantre amesema kuwa timu yake haina budi kufanya vizuri katika mashindano ya Super Cup yanayofanyika nchini Kenya kutokana na ubora na ukubwa wa timu ya Simba.
 
Kocha huyo amesema hayo leo Juni 3, 2018 katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mchezo wa mashindano hayo dhidi ya Kariobangi Sharks siku kesho Juni 4, 2018 na kuongeza licha ya changamoto ya majeruhi na kuchelewa kwa wacheazaji wake lakini ni lazima timu ioneshe kiwango bora na kushinda taji.
“Nimekuwa nikiwaambia wachezaji kwamba wanapaswa kuwa na motisha kubwa kushiriki michuano hii, na unajua baadhi ya awachezaji walikosekana kutokana na sababu mbalimbali na kuna wachezaji wengine wawili walikuwa ni majeruhi lakini tunapaswa kuheshimu jina la Simba kwa kuhakikisha tunaonesha kiwango bora katika mashindano haya” amesema Lechantre
Kocha huyo ameongeza kuwa atabadili mfumo wa uchezaji kutokan na changamoto ya wachezaji kuchelewa kuwasili kujiunga na timu na kusema kuwa itachukuwa muda kwa wachezaji hao kuzoea mfumo huo hasa katika weneo la ushambuliaji.
Leo Juni 3 mpaka 10, 2018 mashindano ya Super Cup yanafanyika mjini Nairobi nchini Kenya kwa kuzikutanisha klabu nane kutoka Tanzania na Kenya, ambapo Tanzania inawakilishwa na vilabu vya Simba, Yanga, Singida United na JKU kutoka Zanzibar na kwa upande wa Kenya ni Goh Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz

No comments:

Powered by Blogger.