Header Ads

Okwi atapona kabla ya kuwavaa Waarabu ?

Baada ya jana kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi anaendelea vizuri na atarudi dimbani mapema kutokana na matibabu anayopata.

Akiongea leo daktari wa timu ya Simba Yassin Gembe amesema, ''Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana atacheza michezo ijayo'', amesema.
Gembe ameongeza kuwa kwa ilivyo hali ya Okwi atakuwa tayari kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Stand United siku ya Ijumaa, Februari 2 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, pamoja na mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry Februari 6.


Okwi aliumia jana kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC uliopigwa kwenye uwanja wa taifa, ambapo alikuwa tayari ameshafunga mabao mawili na kusaidia moja katika ushindi wa mabao 5-0 iliopata Simba.
Okwi ambaye ni raia wa Uganda amesajiliwa msimu huu na Simba akitokea Sports Club Villa na tayari ameshaifungia Simba mabao 16 hivyo kuwa kinara wa mabao hadi sasa kwenye ligi kuu.

No comments:

Powered by Blogger.