Zidane amtupa nje Ronaldo
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemwacha nje ya kikosi nyota wa
timu hiyo Cristiano Ronaldo kitakachocheza leo usiku dhidi ya Espanyol
kwenye La Liga.
Zidane
amesema Ronaldo hatacheza kwasababu ameamua kumpumzisha. Mapumziko hayo
aliyopewa Ronaldo na yametafsiriwa kama kumuacha asubiri mchezo wa Ligi
ya Mabingwa dhidi ya PSG Machi 6.
Hii ni mara ya pili sasa ndani ya mechi tatu Ronaldo kupumzishwa ambapo Zidane alifanya hivyo katika mechi ya ligi kuu katikati ya wiki iliyopita dhidi ya Leganes.
Kutokana na Mreno huyo kupumzika, nafasi yake huenda akaanza nyota mwingine Marco Asensio, kuungana na Gareth Bale pamoja na Karim Benzema kwenye safu ya ushambuliaji.
Real Madrid itasafiri katikati ya juma lijalo hadi nchini Ufaransa kwenye mchezo wa UEFA dhidi ya PSG huku ikiwa mbele kwa mabao 3-1 iliyoyapata kwenye uwanja wake wa Santiago Bernabeu.

No comments: