Header Ads

POLISI KENYA MATATANI

 Chombo cha kujitegemea cha kuchunguza shughuli za Polisi nchini Kenya kimeunda Timu kwa ajili ya kuchunguza mauaji ya kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu aliyepigwa risasi jana.
Mamlaka hiyo Huru ya Kusimamia shughuli za Polisi (IPOA) imesema, imepeleka haraka kikosi hicho kwa ajili ya kuchunguza mauaji hayo ya Evans Njoroge, aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Meru.
Kiongozi huyo wa wanafunzi aliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wakati wa maandamano ya kupinga upandishwaji wa ada pamoja na hali mbaya ya chuo.
Vyombo vya habari vya ndani vimewanukuu mashuhuda wakisema, kiongozi huyo wa wanafunzi alikuwa akikimbizwa na polisi kabla ya kumpiga risasi.
Hadi sasa Polisi wahajazungumzia lolote kuhusiana na tukio hilo.
Katika mitandao ya kijamii, kumekuwepo na kipande cha video kinachomuonesha kiongozi huyo akiwahimiza wenzake kupambana kwa ajili ya kudai haki.

No comments:

Powered by Blogger.