Header Ads

Yanga yapewa Burundi, Simba Afrika Kusini

Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa kati ya Yanga na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6, 2018 Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.

CAF pia imewataja waamuzi kutoka Afrika Kusini kuchezesha mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Simba dhidi ya Al Masry ya Misri Februari 7 kwenye uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni.
Waamuzi wa mchezo wa Yanga ni, Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana na wasaidizi wake Willy Habimana na Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo ni Mangaluso Jabulani Langwenya kutoka Swaziland
Kwa upande wa Simba ni Mwamuzi wa kati Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena, Athenkosi Ndongeni pamoja na Christopher Harrison huku kamishna akiwa ni Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.
 Mechi ya marudiano kati ya Yanga na Township Rollers FC  itachezwa Machi 17, 2018 nchini Botswana, ikichezeshwa na waamuzi kutoka Morocco. Kwa upande wa Simba mechi yao ya marudiano itapigwa huko Port Said Misri Machi 17, 2018 ikichezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea.

No comments:

Powered by Blogger.