Barnaba awavuruga
Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic'
amefunguka na kurusha jiwe gizani kwa kusema hakuna kitu ambacho anaweza
kuwalipa watu waliomtendea mema na hata mabaya mpaka kufikia sasa
alipo.
Barnaba
ametoa kauli hiyo kwenye ukurasa wake maalumu wa kijamii mchana wa leo
baada ya kile kinachodaiwa na watu wengi huenda maneno hayo aliyoyatoa
bado yanamlenga mzazi mwenzake mama Steve 'Zuu Namela' kutokana na
kutengana kwako huku wengine wakidai huenda ni mashairi ya wimbo uliopo
katika albamu yake anayotarajia kuiachia hivi karibuni.
"Ukimtumainia yeye kila kitu kitaenda sawa tumpe sifa na utukufu Mungu wetu aliyejuu 'major day' na tujifunze kusamehe haraka na kutoa tulivyonavyo moyoni ili tuwe na nafasi kubwa kwenye milango ya mbingu. Hakuna kitu naweza kulipa kwa mlionitendea mema na kwa watenda mabaya, zaidi ya Mungu pekee. Mimi ni mwenye kutambua thamani ya kila aliyepandikiza nguvu ndani ya kipaji changu 'so' sina budi kusema asante mungu kwa kuniweka adi Leo", amesema Barnaba.
Kwa upande mwingine, msanii Barnaba amesema anajisifu kwa sauti yake ambayo kwa sasa imekua sehemu ya burudani au nusu chakula juu ya muziki wake.

No comments: