Alichokisema Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kuhusu Serikali Kuwafungia Wasanii
“Viongozi
wanaoshughulika na masuala ya sanaa na utamaduni wasiifanye kazi hii
kama kazi ya uhakimu bali waifanye kama kazi ya Ualimu kwa kuwafundisha
watu namna ya kufanya”- amesema James na kuongeza;
“Serikali
ya CCM imeahidi ajira kwa vijana, Vijana wameamua kujiajiri kwenye
sanaa. Walimu wetu ni kuwawezesha kwenye sanaa na sio kuwakatisha tamaa
kwahiyo tusitumie kigezo cha sheria na taratibu kuwaangamiza watu ambao
tungeweza kuwaelimisha na wakafanya vizuri zaidi.
“Leo
tuna wasanii ambao wameitangaza nchi yetu vizuri na wanalipa kodi kwa
kazi zao sasa leo tunakwenye kupoteza mabalozi wazuri na walipakodi kwa
makosa madogo ambayo yanaweza kurekebishwa na tukaendelea kufanya
vizuri. Kama tutaaendelea kuwaacha vijana wakiangamizwa kwa kitu
kinaitwa kanuni na taratibu za sheria basi hakuna kijana atakayebaki
hapa”

No comments: